Na VOINA MAGANDA
Jumuiya
ya umoja wa wazazi ni chombo kinachoongozwa na chama cha Mapinduzi, imeundwa
kwa mujibu wa katiba ya Chama Cha Mapinduzi, ya mwaka 1977 Toleo la mwaka 2012
sehemu ya nne ibara ya 129 (1c), 3,4, na 5.
Hii ni
taarifa ya utendaji inayohusu utekelezaji wa ilani ya Chama Cha Mapinduzi
katika Jumuiya ya wazazi pamoja na idara ya Elimu, Malezi na Mazingira kuanzia
Januari mpaka Desemba 2018.
HISTORIA FUPI YA KATA YA MBURAHATI
Mburahati ni eneo la kiutawala ndani
ya wilaya ya Ubungo lenye jumla ya wakazi 34,123 kulingana na sensa ya mwaka
2012 japo kuna kadirio la ongezeko la watu kwa asilimia 5%.
Mburahati ni moja ya kata 14
zinazopatikana katika wilaya ya Ubungo yenye ukubwa wa kilimita za mraba 1.3,
pia ina serikali za mtaa tatu ambazo zote ipo chini ya Chama Cha Mapinduzi.
Mitaa hiyo ni:
1. Serikali ya mtaa Barafu (ina matawi
mawili la Barafu na Darajani)
2. Serikali ya mtaa NHC
3. Serikali ya mtaa Kisiwani.
MIPAKA
Kigeografia Kata yetu ya Mburahati iko
Kama ifuatavyo:-
·
Kusini
imepakana na Kata ya Kigogo (Manispaa ya Kinondoni)
·
Kaskazini
imepakana na Kata ya Makulumla
·
Mashariki
imepakana na Kata ya Mzimuni (Manispaa ya Kinondoni)
·
Magharibi
imepakana na Kata ya Mabibo
UTAWALA WA JUMUIYA YA WAZAZI
UONGOZI
WA KATA
1. JOHN E. MAPUNDA – MWENYEKITI KATA
2. SOPHIA KIROBOTO – KATIBU KATA
3. CHARLES A. KYALAWA - EMMA
KAMATI
YA UTEKELEZAJI KATA
1. BAKARI AMIRI – MJUMBE MKUTANO MKUU MKOA
2. FLORA LWAMBO – MJUMBE HALMASHAURI
KUU KATA
3. RAMADHANI KISHOKA – MJUMBE
HALMASHAURI KUU KATA
4. HUSNA JUMA – MJUMBE
5. SALUMU WINDA – MJUMBE
6. REHEMA MBARAKA – MJUMBE
7. JUMA DADI - MJUMBE, MWAKILISHI UVCCM
8. AMINA YAKUBU – MJUMBE , MWAKILISHI
UWT
9. DOTTO MATHIAS - MJUMBE
10. CATHERINE PAUL- MJUMBE
UONGOZI
WA MATAWI
Kata ya Mburahati ina matawi manne
ambayo uongozi wake uko kama ifuatavyo:
a.
TAWI LA BARAFU
Kulikuwa na mapungufu kwenye Uongozi
katika nafasi ya Katibu EMMA, kamati ya utekelezaji wajumbe 3 ambapo uchaguzi
ulifanyika 19/12/2018 mpaka sasa nafasi hizo zimeshajazwa. Uongozi umekamilika
kwa asilimia 100
b.
TAWI LA NHC
Uongozi umekamilika kwa asilimia 100
c.
TAWI LA KISIWANI
Uongozi umekamilika kwa asilimia 100
d.
TAWI LA DARAJANI
Uongozi umekamilika kwa asilimia 100
UHAI
WA JUMUIYA
IDADI
YA WANACHAMA KATIKA MATAWI
Jumuiya ya Wazazi katika kata ya
Mburahati ina wanachama takribani 845, wanaume wakiwa 355 na wanawake 490.
Mchanganuo wa idadi ya wanachama
katika matawi uko kama ifuatavyo:-
Jedwali I: IDADI YA WANACHAMA
NA
|
TAWI
|
IDADI YA WANACHAMA
|
JUMLA
|
|
ME
|
KE
|
|||
1
|
BARAFU
|
110
|
145
|
225
|
2
|
NHC
|
110
|
190
|
300
|
3
|
KISIWANI
|
55
|
95
|
150
|
4
|
DARAJANI
|
80
|
60
|
140
|
JUMLA
|
355
|
490
|
845
|
VIKAO
KATA NA MATAWI
Jedwali II: viko vya Kata
AINA YA KIKAO
|
VIKAO VYA KIKANUNI
|
VIKAO MAALUM
|
VIKAO VYA DHARURA
|
KAMATI TENDAJI
|
3
|
2
|
1
|
KAMATI YA UTEKELEZAJI
|
3
|
2
|
1
|
BARAZA
|
2
|
-
|
-
|
MKUTANO MKUU
|
1
|
1
|
-
|
Jedwali III: Vikao vya Matawi
TAWI
|
KAMATI TENDAJI
|
KAMATI YA
UTEKELEZAJI
|
MKUTANO WA WANACHAMA WOTE
|
MKUTANO
MKUU
|
BARAFU
|
3
|
3
|
2
|
1
|
NHC
|
4
|
4
|
2
|
1
|
KISIWANI
|
4
|
4
|
2
|
-
|
DARAJANI
|
3
|
3
|
2
|
1
|
MPANGO
KAZI 2017 – 2022
1.
Umoja
wa wazazi Kata ya Mburahati unajua kuwa mwaka 2019 na 2020 kuwa ni miaka ya
uchaguzi, 2019 Serikali za Mitaa 2020 uchaguzi mkuu wa Rais, wabunge na
madiwani, hivyo basi umoja wa wazazi utashirikiana kikamilifu na viongozi wake
wote wa matawi, Chama na Jumuiya nyingine za UVCCM na UWT, Kuhamasisha wananchi
hasa wana CCM kushinda chaguzi zote hizo. Lengo la CCM ni kushika dola katika
ngazi zote.
2. Jumuiya ya Wazazi imedhamiria
kuhakikisha Chama chake cha wananchi cha kuweka na kukupo kinakuwa na kufungua matawi
ndani ya wilaya ya Ubungo na hatimaye mkoa wote. Kwani ni faraja kufikia hatua
ya kuhudumia mkoa huu wa Dar es Salaam ili kukuza mitaji ya wajasiamali kutoka
katika hatua waliyopo kuwa wajasiliamali wa kati.
Ili
kufanikisha hilo tutahakikisha semina za mara kwa mara zinatolewa na Benki na
wataalamu wa Biashara ili kuwajengea uwezo katika utumiaji wa mikopo
watakayokuwa wanachukua na hatimaye waweze kuweka akiba.
3. Ili kutuweka pamoja tutatumia
matamasha ya michezo na ligi za kata ili wanachama na wananchi wa Mburahati
tuongee lugha moja, maana michezo ni afya, furaha pia hujenga mahusiano ushirikiano
baina na mtu na mtu.
4. Kushirikiana na viongozi wa kata
zingine kuanzisha mfuko wa Elimu ya Ufundi ambao utasaidia kupambana na tatizo
zima la ajira kwa vijana wetu badala ya kusubiria kuajiliwa. Maana ujuzi pekee
ndio nyenzo kuu ya kuwa na viwanda vidogo vidogo katika jamii zetu.
IDARA
YA ELIMU, MALEZI, MAZINGIRA NA UCHUMI
1.
Elimu
Kata
ya Mburahati ina shule za awali, msingi na sekondari.
Shule za awali
Shule
za awali ziko 19 lakini katika hizo iliyosajiliwa ni shule moja tu. Zingine
hazijasajiliwa japo zinapokea watoto kutokana na kutokuwa na sifa za kusajiliwa
kama shule za awali japo zinatoa huduma za shule za awali tofauti na taratibu
za wizara ya Elimu na mafunzo ya ufundi, kwa hadhi zinastahili kuwa vituo vya
malezi ya watoto.
Shule za msingi
Shule
za msingi ziko tano (5) ambapo shule nne (4) ni za serikali na shule moja (1)
ni ya binafsi.
Mwaka
2018 Kata ya Mburahati imeshuka kwa asilimia 5.189 ya waliofaulu kwenda
sekondari kuliko mwaka uliopita. Ambapo mwaka 2017 ufaulu ulikuwa 85.468% wa
waliondikishwa kufanya mtihani.
Hata
hivyo idadi ya watahiniwa imeongezeka kwa asilimia 9.127% ambayo ni sawa na
wanafunzi 50 kwa mwaka huu.
Jedwali IV: SHULE, IDADI YA
WATAHINIWA, WALIOFAULU NA WALIOSHINDWA 2018
NA
|
SHULE
|
WALIOANDIKISHWA
|
WALIOTAHINIWA
|
WALIOFAULU
|
SAWA NA ASILIMIA %
|
1
|
Mburahati
|
194
|
194
|
131
|
69%
|
2
|
Barafu
|
141
|
141
|
118
|
84
|
3
|
Bryceson
|
164
|
164
|
144
|
88
|
4
|
Muungano
|
57
|
55
|
49
|
86
|
5
|
A.H
Mwinyi
|
19
|
19
|
18
|
95
|
575
|
573
|
460
|
80.279
|
Jedwali V: SHULE, IDADI YA
WATAHINIWA, WALIOFAULU NA WALIOSHINDWA 2017
NA
|
SHULE
|
WALIOANDIKISHWA
|
WALIOTAHINIWA
|
WALIOFAULU
|
SAWA NA ASILIMIA %
|
1
|
Mburahati
|
202
|
202
|
149
|
73.762
|
2
|
Barafu
|
95
|
95
|
95
|
100
|
3
|
Bryceson
|
122
|
122
|
108
|
88.524
|
4
|
Muungano
|
73
|
73
|
65
|
89.041
|
5
|
A.H
Mwinyi
|
31
|
31
|
30
|
96.774
|
523
|
523
|
447
|
85.468
|
Shule za sekondari
Shule
za sekondari zilizopo katika kata ya Mburahati ni moja tu ya serikali.
Katika
hali inayoumiza shule za serikali zimekuwa na matokeo mabaya sana kuliko shule
ya binafsi maana zimezalisha zero nyingi kuliko waliofaulu kama inavyoonekana
katika jedwali kwa miaka miwili mfululizo.
Jedwali VI : SHULE ZA SEKONDARI NA
MATOKEO YA 2016/2017
NA
|
SHULE
|
2016
|
2017
|
ANGALIZO
|
1
|
Mburahati
S4480
|
DIV
I- 0
DIV
II- 06
DIV
III- 15
DIV
IV- 38
DIV
O- 97
|
DIV
I- 2
DIV
II- 4
DIV
III- 22
DIV
IV- 91
DIV
O- 73
|
JAPO
ZIRO ZIMEPUNGUA LAKINI BADO HALI NI MBAYA SANA
|
Library:
Tumefanikiwa
kuwa na library moja katika kata yetu ambayo hata hivyo vitabu vilivyomo
havitoshelezi mahitaji ya walengwa na kusababisha itumike na watu wachache.
2. Afya:
Kata
ya Mburahati haina Hospitali hata moja, kuna Zahanati nne (4) zinazomilikiwa na
watu binafsi na kituo cha afya kimoja cha serikali na maabara tatu zote za watu
binafsi.
Aidha
kuna jumla ya maduka ya dawa mawili (2) ambayo yamesajiliwa na yamekidhi
vigezo. Japo kuna maduka ya dawa mengi katika maeneo yetu lakini ni jambo la
kusikitisha kuwa hayana usajili wa mamlaka zinazohusika.
Idara
ya afya kwa kushirikiana na idara ya Elimu, ilifanikiwa katika zoezi la utoaji
wa chanjo za magonjwa yasiyopewa kipaumbele kama Usubi, minyoo ya tumbo,
ngirimaji, matende, na kichocho kwa wanafunzi wa shule za msingi za serikali na
binafsi.
Zoezi
hilo limerudiwa mwezi huu tokea Jumamosi ya tarehe 15-20 katika ofisi za
Serikali ya mtaa. Pamoja na changamoto ndogo ndogo zilizojitokeza wakati wa
utekelezaji wa zoezi hilo waliweza kufanikiwa kuzitatua.
Bima ya Afya
Wazee
357 wamepewa kadi za bima ya Afya na 49 wamejiandikisha katika Bima ya afya
kupitia serikali za mtaa wanaoishi ili kupata huduma ya matibabu na kufanya
jumla ya wazee 406 walioandikishwa.
Hata
hivyo jumuiya ya wazazi tunaendelea kuwasisitiza wazee wajiandikishe ili wapate
huduma ya matibabu inayotolewa na serikali kwa ajili yao.
3.
Mazingira
Mitaa
yote ina mkandarasi wa uzoaji taka aliepitishwa katika vikao vya serikali ya
mtaa na wastani wa taka ambazo zimeondolewa mpaka sasa ni zaidi ya tani 4660. Maeneo
mengine yanasafishwa na wananchi wenyewe hasa wafanyabiashara ambapo siku ya
jumamosi ni siku ya usafi wa jumla.
Pamoja
na hayo lakini bado usafi umekuwa ni changamoto katika maeneo ya skwata, ikichangiwa
sana na tabia halisi za wakazi ambao hawajali namna za kutunza taka, baadhi
hutupa taka njiani.
Miundombinu
ya barabara pia imeleta shida kwa baadhi ya maeneo na kusababisha magari
makubwa ya taka kushindwa kufika hivyo kufanya zoezi la uzoaji taka kusua sua.
Upandaji miti
Ili
kuboresha mazingira yetu miti 11 ilipandwa ambapo miti saba (7) ni ya matunda
na miti minne (4) ya kivuli mpaka sasa iliyohai ni miti tisa (9) tu.
4.
Uchumi
Mnamo
februari 20, 2018 Jumuiya wa wazazi kata ya Mburahati ilifanikiwa kuanzisha
chama cha akiba na mikopo “WAZAZI
MBURAHATI SACCOS” ambacho kinasimamiwa na kuongozwa na Jumuiya ya Wazazi ya
Mburahati. Haikuwa kazi rahisi katika kulifanikisha hili. Ni juhudi za
wanachama, Uongozi wa Mkoa, Wilaya pamoja na jumuiya ambazo zilileta matokeo
chanya.
Uzinduzi
ulifanywa na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Mkoa Komredi Frank Kamugisha.
Hapo
kabla Jumuiya haikuwa na mradi wowote wa kuifanya jumuiya ijiendeshe kiuchumi
na kufanya viongozi wagharamie wenyewe shughuli zote zitokanazo na jumuiya.
Mikopo
Mpaka
sasa SACCOS imefanikiwa kuwa na wanachama 205, lakini walio hai ni 119 na mmoja
amejitoa kulingana na sababu ya kutokidhi vigezo tulivyoviitaji.
Chama
bado hakijaanza kutoa mikopo maana hakuna mwanachana aliyefikia sifa za kupata
mkopo.
Baadhi
ya sifa ni kuwa na Hisa 5 na kuendelea, kuweka akiba 30% ya mkopo utakaoomba na
kuwa mkazi wa wilaya ya Ubungo, japo ni kusudio letu kuhudumia mkoa mzima
lakini tuliona ni busara kuanza na wilaya ya Ubungo kwanza mpaka mtaji
utakapokua.
Uongozi
wa SACCOS umeanza mazungumzo na Banki ya Posta ili kupata fedha za kukopesha
wananchi na benki imetutaka kuhamasisha wananchi wajiunge kwenye vikundi vya
ujasiriamali, wajisajili kwenye SACCOS ili wapatiwe elimu ya biashara kabla ya
kupewa mikopo. Mchakato huo umeshaanza.
Tukumbuke
kwamba SACCOS imeanzishwa na Jumuiya ya Wazazi lakini inasimamiwa na sheria za
fedha za Tanzania chini ya vyama vya Ushirika kwa muongozo wa Banki kuu.
Kwenye
mikopo ya Manispaa vikundi 63 vimesajiliwa kutoka katika mitaa mitatu ambayo ni
Barafu vikundi 14, kisiwani 12, NHC 37. Mpaka sasa ni vikundi 35 vilivyojaza
fomu za kuomba mikopo na zilizorudishwa ni fomu 22 tu na vikundi 19 ndivyo
vilivyopendekezwa kupewa mikopo katika awamu ya kwanza, jumla ya Tshs
125,000,000/= inatarajiwa kukopeshwa kwa wanachama 283 wa vikundi hivyo.
Bado
elimu ya mikopo inaendelea kutolewa na maafisa toka benki husika ili kuwajengea
uwezo wakopaji wa pesa hizo.
Shughuli zingine:
1. Machi 24, uongozi na wanachama wa
jumuiya ya wazazi waliadhimisha wiki ya wazazi kwa kutembelea zahanati ya kata
ya Mburahati kwa kufanya usafi maeneo yanayoizunguka zahanati hiyo.
Siku
hiyo viongozi mbalimbali wa wilaya na kata walishiriki zoezi hilo wakiongozwa
na Mh. Diwani wa kata ya Mburahati, mwenyekiti wa wazazi wilaya, katibu wa EMMA
wilaya, viongozi wa chama Mburahati, na wanachama wa chama cha Mapinduzi.
2.
Agusti
2018 jumuiya ya wazazi ikishirikiana na Bodi ya WAZAZI MBURAHATI SACCOS waliandaa
ligi ya mpira wa miguu ikishirikisha vijana wa mitaa yote mitatu lengo likiwa
ni kuitangaza jumuiya ya wazazi na SACCOS, huku wakiwa na kauli mbiu ya SIASA
NA UCHUMI. Mgeni rasmi alikuwa mkuu wa wilaya Kisale Makoli.
Ligi
ilichezwa kwa muda wa wiki mbili, mbali na lengo kuu, pia tulikusudia kuundwa
kwa timu ya kata ambayo itakuwa inashiriki michuano katika ngazi ya wilaya.
3.
Jumuiya
ya wazazi imekusudia kutembelea kituo cha watoto wenye mahitaji na kuwapa
zawadi siku ya tarehe 29/12/2019. Kupanda miti katika zahanati ya Mburahati ili
kufanya mazingira ya kata yetu kuboreka zaidi.
Mafanikio
1. Elimu imeendelea kutolewa bila
malipo kwa kufanya ongezeko la wanafunzi kuwa kubwa zaidi ya idadi
iliyotarajiwa hiyo yote imetokana na dhamira ya kweli ya serikali kuu kuhakikisha
kila mtoto wa Mtanzania anapata haki ya kikatiba ya kupata elimu bila kikwazo
chochote. “ELIMU BURE”.
2. Huduma ya Msamaha wa matibabu kwa wazee
haijabagua itikakadi wala dini kwa wanufaika
3. Tumefanikiwa kusajili na kuzindua na
chama cha wananchi cha kuweka na kukopa (saccos).
4. Kuendesha ligi ya kata na kutoa
zawadi ya Jezi seti mbili na mipira saba, tshirt za jumuiya ya wazazi na zenye
maandishi ya SACCOS na kauli mbiu “michezo na uchumi” ili kuhamasisha vijana na
wananchi.
5. Kupanda miti ya kivuli na matunda
6. Kushiriki katika usafi wa mazingira
na wanachi wengine Jumuiya ya wazazi
7. Kata ya Mburahati ilishiriki
kikamilifu kuhakikisha Chama cha Mapinduzi kinashinda kwenye chaguzi za marudio
zilizofanyika jimbo la Kinondoni na Ukonga.
Changamoto
Elimu
1. Watoto kulelewa na mzazi mmoja
2. Utoro kwa wanafunzi
3. Uzembe na uvivu wa wazazi kufuatilia
maendeleo ya mtoto kitaaluma
4. Wingi wa wanafunzi darasani
5. Upungufu wa walimu wa sayansi na
hisabati
6. Upungufu wa vitabu
7. Upungufu wa vyumba vya madarasa na
nyumba za walimu
8. Uchakavu wa majengo na paa (shule za
msingi)
9. Baadhi ya wanafunzi kumiliki simu na
hata kwenda nazo shule hasa
wanafunzi wa sekondari
Mfano:
Taarifa
za mwanafunzi wa kidato cha pili shule ya sekondari
Mburahati, kutofika shule na badala yake kwenda kwenye mageto ya vijana. Mzazi
naligundua hilo lakini hakutoa taarifa Polisi.
Afya
1. Mpaka kufikia tarehe 17/12/2018
zaidi ya wazee 49 hawajachukua kadi zao za msamaha wa matibabu katika ofisi za
Afisa mtendaji jambo ambalo linaweza kutafsiriwa kuwa linatokana na mawasiliano
duni kati ya viongozi wenye dhamana na wananchi.
2. Huduma ya afya haitoshelezi idadi ya
watu waliopo katika kata ya Mburahati, hivyo hitaji la hospital na vituo vya
afya ni kubwa
3. Bado kuna malalamiko kuhusu
ufuatiliaji wenye nyumba wasiojengea mashimo ya choo, na kutiririsha maji
machafu ambayo ni hatari na yanaweza kusababisha magonjwa ya mlipuko.
4. Idadi ya maduka ya dawa ni mengi
lakini yaliyosajiliwa ni mawili hivyo kuhatarisha afya za wakazi wa eneo hili.
Uchumi
1. Mitaji duni ya wafanyabiashara wengi
huchangia biashara zao kufa
2. Uelewa duni wa utafutaji masoko na elimu ya biashara kwa
ujumla linachangia kuzorota kwa uchumi wa familia
Utawala
1. Matatizo tuliyonayo katika Kata yetu
kutokuwa na Ofisi ya kujitegemea ya Kata hata matawi kama jumuiya.
Mapendekezo:
1. Ili kutatua na kumudu kushughulikia
kero ni lazima maafisa wa serikali wawe na utayari na uelewa wa sheria
zinazolinda haki ya mtoto katika jamii ili kutoyafumbia macho maovu kwa
kisingizio cha kukosa ushirikiano wa wazazi na jamii, maana sheria iko wazi
kuhusu uwajibishwaji kwa mtuhumiwa mara anapobainika kuwa na kosa.
2. Ni muhimu kwa viongozi wa chama
ambao tunaisimamia serikali katika utekelezaji wa ilani kuwa mstari wa mbele
kukemea na kuhakikisha sheria inafuata mkondo wake huku tukihamasisha wananchi
kufuatilia haki zao za msingi kuliko kulalamika.
3. Wazazi Mburahati Saccos iangaliwe
kwa jicho la pekee, ili halmashauri ya Ubungo ifikirie kutumia Saccos hii
kukopesha vikundi vya wananchi badala ya kupeleka kwenye mabenki, maana hatua
hiyo itaziwezesha saccos kuwa na uwezo zaidi.
4. Chama cha Mapinduzi ikumbuke kutoa
asilimia kwa jumuiya ya wazazi maana tuna mradi wa mnara Barafu, mradi wa kukodisha
fremu na kuna uwekezaji wa jengo na sheli ya mafuta ambapo mapato yake
yanalipwa lakini jumuiya hii imesahaulika na kuifanya ijiendeshe kwa
kujichangisha.
MALENGO
1. Jumuiya ya wazazi kwa kushirikiana
na viongozi wa kata zingine imekusudia kuwa na mfuko wa Elimu ambao utanufaisha
vijana waliohitimu elimu ya sekondari na kushindwa kujiendeleza katika chuo cha
ufundi VETA
2. Kuunganisha wanachama na Saccos ya
Mburahati na hatimaye kuwa na matawi ili kujenga umoja baina ya Jumuiya za
wazazi kata na kata, hatimaye wilaya, na mkoa.
3. Kuanzisha ligi ya mpira wa miguu
ambayo itajumuisha jumuiya ya wazazi ya kata zingine ndani ya wilaya ya Ubungo
ikiwa na lengo la kutuweka wana CCM pamoja na kufahamiana.
HITIMISHO: Mungu isaidie Kata ya
Mburahati na kazi za mikono yetu.
IMETHIBITISHWA NA KAMATI YA UTEKELEZAJI YA
BARAZA KUU LA WAZAZI KATA YA MBURAHATI
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni