Wanaofuata

Ijumaa, 28 Desemba 2018

TAARIFA YA UTENDAJI YA MWAKA 2018: KATA YA MAKUBURI


na VOINA MAGANDA 

UTANGULIZI 
Jumuiya ya wazazi Kata ya Makuburi ni moja ya Jumuiya za CCM
inayojumuisha Kata (14) ndani ya Wilaya ya Ubungo.
A.  MIPAKA
Kihistoria Kata yetu ya Makuburi Kama ifuatavyo:-
·      Kusini imepakana na Kata ya Tabata Kimanga Wilaya ya Ilala
·  Mashariki imepakana na Kata ya Mabibo Wilaya ya Ubungo.
·  Magharibi imepakana na Kata ya Kimara Wilaya ya Ubungo
·  Kaskazini imepakana na Kata ya  Ubungo Wilaya ya Ubungo


C.  IDADI YA WATU
Kwa mujibu wa senza ya mwaka 2012 idadi ya watu ni kama ifuatavyo:-
MTAA
KAYA


MWONGOZO
2884


14194
MAK/KIB
2329


11156
KIBANGU
3071


15610
KAJIMA
1589


7322
MAKOKA
1794


9126
JUMLA
11,667


57,408
2.   UONGOZI WA KATA
1.    VICENT MGOGORO – MWENYEKITI KATA
2.    ALLY HASSAN SEMBOGA – KATIBU KATA
3. VOINA MAGANDA -  KATIBU EMMA KATA

KAMATI YA UTEKELEZAJI KATA

1.    ABEL NGOFILO – MJUMBE HALMASHAURI KUU KATA
2.    EMMANUEL NYANGOI – MJUMBE
3.    ANDREW MWAMASANGULA – MJUMBE
4.    NEZERINA BOMA – MJUMBE, ANATUWAKILISHA MKOA
5.    HERIETH NGINDO – MJUMBE
6.    SHABAN CASTO -  MJUMBE, MWAKILISHI UVCCM
7.    ANNAGORETH MANAMBA – MJUMBE , MWAKILISHI UWT

3.   UONGOZI WA MATAWI
1.   TAWI LA MIKONGENI
Uongozi umekamilika kwa asilimia 100

2.   TAWI LA MWONGOZO
Viongozi hawajakamilika na hata aliyekuwa Katibu Tawi hili ameandika barua ya kujiuzuru. Barua hiyo nimeipokea tarehe 22/11/2018.
Zipo nafasi mbalimbali zinatakiwa zijazwe

3.   TAWI LA MABIBO KIBANGU
Kuna nafasi ziko wazi na pia wameleta muhtasari wao unaoomba kuwa kuna baadhi ya viongozi hawapo tayari kuendelea kwa sababu mbalimbali zikiwemo kuwa na nafasi zaidi ya moja, umri na kadhalika.

4.   TAWI LA UBUNGO KIBANGU
Taratibu za uchaguzi zinaendelea, fomu zinatolewa kwa wanaotaka kugombea hapo karibu nafasi zote wengi walikuwa na nafasi mbili.


5.   TAWI LA CITY VIEW
Viongozi wote wamekamilika na wanachapa kazi

6.   TAWI LA KAJIMA
Viongozi wote wamekamilika wanachapa kazi

7.   TAWI LA MAKOKA A
Halina uongozi nafasi zote zimetanganzwa upya, fomu zimetolewa na wanachama wamejitokeza kujaza taratibu nyingine zinaendelea.

8.   TAWI LA MAKOKA B
Viongozi wapo ila katibu wa EMMA wa Tawi hilo ni balozi amesema anaachia ukatibu EMMA Taratibu za uchaguzi zinaendelea

4.   UHAI WA JUMUIYA
A.  IDADI YA MATAWI
Kata ya Makuburi ina matawi manane (8)
1.    Mikongeni
2.    Mwongozo
3.    Mabibo kibangu
4.    Ubungo kibangu
5.    City view
6.    Kajima
7.    Makoka A
8.    Makoka B

  

B.   IDADI YA WANACHAMA
Idadi ya wanachama katika matawi ni kama ifuatavyo:-
NA
TAWI
IDADI YA WANACHAMA
JUMLA
WALIOHAI
JUMLA
ME
KE
ME
KE
1
UBUNGO KIBANGU
43
60
103
30
38
68
2
CITY VIEW
102
158
250
69
91
160
3
MWONGOZO
59
116
177
32
60
92
4
MIKONGENI
58
64
132
31
38
67
5
KAJIMA
54
56
110
20
15
35
6
MAKOKA A
51
56
107
27
35
62
7
MAKOKA B
84
206
290
63
92
155
8
MAKUBURI KIBANGU
61
50
111
39
44
83
JUMLA
403
766
1169
311
369
680

C.  VIKAO KATA NA MATAWI
NGAZI YA KATA
JEDWALI
AINA YA KIKAO
VIKAO VYA KIKANUNI
VIKAO MAALUM
VIKAO VYA DHARURA
KAMATI TENDAJI
2
-
-
KAMATI YA UTEKELEZAJI
2
-
5
BARAZA
1
-
-
MKUTANO MKUU
1
-
-



NGAZI YA MATAWI
JEDWALI
TAWI
KAMATI TENDAJI
KAMATI YA
UTEKELEZAJI
MKUTANO WA WANACHAMA WOTE
MKUTANO
MKUU
MIKONGENI
1
3
-
-
MWONGOZO
-
4
1
-
MAK/KIBANGU
-
4
-
-
UB/ KIBANGU
-
-
-
-
CITY VIEW
-
2
-
-
KAJIMA
-
5
-
-
MAKOKA A
-
-
-
-
MAKOKA B
-
-
-
-

5.   MPANGO KAZI 2017 – 2022
Umoja wa wazazi Kata ya Makuburi unajua kuwa mwaka 2019 na 2020 kuwa ni miaka ya uchaguzi 2019 Serikali za Mitaa 2020 uchaguzi mkuu wa Rais, wabunge na madiwani, hivyo basi umoja wa wazazi utashirikiana kikamilifu na viongozi wake wote wa matawi pia kwa kushirikiana na viongozi wote wa Chama na Jumuiya nyingine za CCM UVCCM na UWT, Kuhamasisha wananchi hasa wana CCM kushinda chaguzi zote hizo.

6.   ELIMU/ MALEZI NA MAZINGIRA 
Elimu 
Kata ya Makuburi ina shule za awali, msingi na sekondari. 

Shule za awali 
Shule za awali hakuna iliyosajiwa hata moja kutokana na kutokuwa na
sifa za kusajiliwa kama shule za awali japo zinatoa huduma za shule za
awali tofauti na taratibu za wizara ya Elimu na mafunzo ya ufundi, kwa
hadhi zinastahili kuwa vituo vya malezi ya watoto.

Shule za msingi 
Shule za msingi 11ambapo shule sita (6) ni za serikali na shule tano (5) ni za binafsi.

Mwaka 2018 Kata ya Makuburi imeshuka kwa asilimia 1.644 ya waliofaulu kwenda sekondari kuliko mwaka uliopita. Ambapo mwaka 2017 ufaulu ulikuwa 93.816% waliandikishwa wanafunzi 946  waliofanya mtihani ni 938 na waliofaulu walikuwa 880.

Idadi wa wanafunzi waliofanya mtihani wa darasa la saba ni 856 kati ya 857 na waliofaulu ni 789 sawa na asilimia 92.172% ya wanafunzi wote waliomaliza elimu ya msingi kwa mwaka wa masomo 2018.

Aidha shule moja ya binafsi ilisajiliwa na kufanya idadi ya shule za msingi ziwe 11 badala ya 10 zilizokuwepo mwaka 2017.

Hata hivyo idadi ya watahiniwa imepungua kwa asilimia 18.976% ambayo ni sawa na wanafunzi 178.

Jedwali III: SHULE, IDADI YA WATAHINIWA, WALIOFAULU NA WALIOSHINDWA 2018
NA
SHULE
WALIOANDIKISHWA
WALIOTAHINIWA
WALIOFAULU
SAWA NA ASILIMIA %




1
MAKUBURI
119
119
111
90.48
2
MAKOKA
250
250
212
84.8
3
MABIBO
96
96
91
94.79
4
MAKUBURI JESHINI
47
47
47
100
5
KIBANGU
68
68
63
96.92
6
MATSAPA
27
27
27
100
7
KIBANGU ENGL
49
49
48
99.5
8
BETHEL MISSION
28
28
28
100
9
UBUNGO KISIWANI
143
142
132
92.30
10
SANTA LUKA
25
25
25
100
11
EMMANUEL
05
05
05
100


857
856
789
92.172


Jedwali IV: SHULE, IDADI YA WATAHINIWA, WALIOFAULU NA WALIOSHINDWA 2017

NA
SHULE
WALIOANDIKISHWA
WALIOTAHINIWA
WALIOFAULU
SAWA NA ASILIMIA %
1
MAKUBURI
125
124
124
100
2
MAKOKA
251
249
203
81.526
3
MABIBO
142
141
135
95.744
4
MAKUBURI JESHINI
52
52
50
96.153
5
KIBANGU
62
62
62
100
6
MATSAPA
22
22
22
100
7
KIBANGU ENGL
75
74
70
94.594
8
BETHEL MISSION
28
28
28
100
9
UBUNGO KISIWANI
170
167
167
100
10
SANTA LUKA
19
19
19
100
11
EMMANUEL
NIL
NIL
NIL
NIL


946
938
880
93.816

Shule za sekondari 
Shule za sekondari zilizopo katika kata ya makuburi ni tatu (3) za serikali zikiwa mbili na ya binafsi moja.

Katika hali inayoumiza shule za serikali zimekuwa na matokeo mabaya sana kuliko shule ya binafsi maana zimezalisha zero nyingi kuliko waliofaulu kama inavyoonekana katika jedwali kwa miaka miwili mfululizo.


Jedwali V : SHULE ZA SEKONDARI NA MATOKEO YA 2016/2017

NA
SHULE
2017
2016
ANGALIZO
1
MAKOKA
S4598
DIV I- 2
DIV II- 20
DIV III- 30
DIV IV- 100
DIV O- 46
DIV I- 2
DIV II- 11
DIV III- 23
DIV IV- 66
DIV O- 87

UFAULU UMEZIDI KUSHUKA
2
YUSUFU MAKAMBA
S1806
DIV I- 0
DIV II- 6
DIV III- 13
DIV IV- 113
DIV O- 68
DIV I- 1
DIV II- 8
DIV III- 23
DIV IV- 108
DIV O- 115

UFAULU UMEZIDI KUSHUKA
3
UBUNGO ISLAMIC
S0671
DIV I- 1
DIV II-24
DIV III-49
DIV IV- 50
DIV O- 0
DIV I- 5
DIV II- 30
DIV III- 54
DIV IV- 34
DIV O- 0

UFAULU UMEONGEZEKA

Afya:
Kata ya Makuburi ina Hospitali moja ambayo inamilikiwa na kanisa Katoliki katika mtaa wa Makoka, kituo cha Afya kimoja kilichopo Mtaa wa Mwongozo, dispensary mbili na maduka ya dawa 14 yaliyosajiliwa na yasiyosajiliwa 61 na kufanya jumla ya 75.

Idara ya afya kwa kushirikiana na idara ya Elimu, ilifanikiwa katika zoezi la utoaji wa chanjo za magonjwa yasiyopewa kipaumbele kama Usubi, minyoo ya tumbo, ngirimaji, matende, na kichocho kwa wanafunzi wa shule za msingi za serikali na binafsi isipokuwa shule ua BETHEL MISSION walikataa kutokana na imani yao. Pamoja na changamoto ndogo ndogo zilizojitokeza wakati wa utekelezaji wa zoezi hilo waliweza kufanikiwa kuzitatua.

Mazingira 
Kata ya Makuburi ina barabara tatu ambazo zinahudumiwa na Halmashauri ya manispaa ya Ubungo nazo ni barabara ya Mandera, Maji Chumvi na ile inayoelekea kwa mzee wa Upako.Maeneo mengine yanasafishwa na wananchi wenyewe hasa siku ya jumamosi ambayo ni ya usafi wa jumla.

Aidha mitaa yote ina wakandarasi wa uzoaji taka waliopitisha katikakikao cha serikali ya mtaa na wastani wa taka ambazo zimeondolewa kwa muda wa miezi tisa ni tani 6723 zilikusanywa kutoka katika matawi yote.

Pamoja na hayo lakini bado usafi umekuwa ni changamoto katika kata ya Makuburi ikichangiwa sana na tabia halisi za wakazi ambao hawajali namna za kutunza taka, baadhi hutupa taka njiani.

Miundombinu ya barabara pia imeleta shida kwa magari makubwa ya taka kufika baada ya maeneo na kufanya kazi ya uzoaji kusua sua.

Upandaji miti 
Ili kuboresha mazingira yetu miti 150 tu ambayo imepandwa mpaka sasa japo iliyohai haizidi miti miti 100 kutokana na uangalizi duni wa miti hiyo, huku maeneo yenye wanyama wa kufuga kuachia mifugo yao ambayo imeharibu miti hiyo.

Bima ya Afya 
Wazee 307 wamejiandikisha katika Bima ya afya kupitia serikali za mtaa wanaoishi ili kupata huduma ya matibabu lakini mpaka sasa kadi ambozo zimechukuliwa ni 163 kati ya zilizoombwa.

Changamoto ilijitokeza na kugundulika baada ya kadi kuanza kugawiwa kwa waliojiandikisha, kuwa kuna baadhi ya kadi zilikosewa kwa kuwa na taarifa za mtu mwingine, jambo hilo linaendelea kufanyiwa kazi kwa kila utakayekuwa na tatizo hilo.

Kwa sababu hiyo iliamuliwa kuwa wazee ambao hawajajiandikisha watakamilisha zoezi hilo katika ofisi za mtaa na wao ndio watapeleka kwa mtendaji wa kata kwa ajili ya taratibu zingine.

Jedwali VI: IDADI YA WAZEE WALIOCHUKUA BIMA KATIKA MTAA
NA
MTAA
TAWI
KADI ZILIZOCHUKULIWA
1
KIBANGU
Ubungo Kibangu
38
City view
2
MAKOKA
Makoka A
10
Makoka B
3
MAKUBURI KIBANGU
Makuburi Kibangu
19
4
MWONGOZO
Mwongozo
83
Mikongeni
5
KAJIMA
Kajima
13


JUMLA

163

Uchumi 
Jumuiya wa wazazi kata ya makuburi haina mradi wowote wa kuifanya jumuiya ijiendeshe kiuchumi na kufanya viongozi wagharamie wenyewe shughuli zote zitokanazo na jumuiya.

Mikopo 
Wananchi 360 walioko kwenye vikundi kwa mikopo waliomba jumla ya Tshs 257,900,000/=, waliohudhuria mafunzo walikuwa  307 ambapo mafunzo yaliyotolewa na maafisa wa Benki ya CRDB kwa ajili ya kuwapa mikopo ya Manispaa. Kati ya hao ni 161 waliokopeshwa jumla ya Tshs 75,000,000/= (million sabini na tano tu) katika awamu ya kwanza.

Wengine walikosa kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo ya katiba, ambavyo katiba 19 zilifanyiwa marekebisho.

Mafanikio:
Elimu imeendelea kutolewa bila malipo kwa kufanya ongezeko la wanafunzi kuwa kubwa zaidi ya idadi iliyotarajiwa
Huduma ya Msamaha wa matibabu kwa wazee haujabagua itikakadi wala dini kwa wanufaika

CHANGAMOTO
Elimu
1.                Utoro kwa wanafunzi
2.                Wingi wa wanafunzi darasani
3.                Upungufu wa walimu wa sayansi na hisabati
4.                Upungufu wa vitabu
5.                Upungufu wa vyumba vya madarasa na nyumba za        walimu
6.                Uchakavu wa majengo na paa (shule za msingi)
7.                Baadhi ya wanafunzi kumiliki simu na hata kwenda nazo           shule hasa wanafunzi wa sekondari
8.                Baadhi ya shule hazina uzio (shule ya sekondari         Makamba, Shule ya msingi Makoka)
9.                Upungufu wa mashimo ya choo kwa shule zote za msingi          na sekondari
10.           Ufaulu duni kwa shule za sekondari unaosababishwa na mambo mbalimbali mfano:  Shule ya Makamba ina       mwalimu mmoja wa Biology
11.           Ushiriano wa wazazi katika kutatua tatizo la unyanyasaji wa mtoto wa kike ni mdogo na wakati mwingine hakuna      kabisa

Mfano:
  • Taarifa za mwanafunzi wa kidato cha tatu shule ya sekondari Makamba, kuishi kinyumba na           mwanaume, wazazi na majirani walikataa kutoa        ushirikiano
  • Mtoto wa darasa la tatu shule ya msingi ya Mabibo alibakwa na kulawitiwa na mtu aliyejiita nabii wa          kanisa lililopo Makoka, afisa ustawi alipolifuatilia alikosa uhirikiano pia.
Afya
1Mpaka kufikia tarehe 30/09/2018 zaidi ya wazee 144 hawajachukuakadi zao za msamaha wa matibabu katika ofisi za Afisa mtendaji jambo ambalo linaweza kutafsiriwa kuwa linatokana na mawasiliano duni kati ya viongozi wenye dhamana na wananchi.
2.    Huduma ya afya haitoshelezi idadi ya watu waliopo katika kata ya makuburi, hivyo hitaji la hospital na vituo vua afya ni kubwa
3.    Bado kuna malalamiko kuhusu ufuatiliaji wenye nyumba wasiojengea mashimo ya choo, na kutiririsha maji machafu ambayo ni hatari na yanaweza kusababisha magonjwa ya mlipuko. 

Uchumi
1.    Mitaji duni ya wafanyabiashara wengi huchangia biashara zao kufa

2.    Uelewa duni  wa utafutaji masoko na elimu ya biashara kwa ujumla linachangia kuzorota kwa uchumi wa familia 

Mapendekezo:
1.    Ili kutatua na kumudu kuhughulikia kero ni lazima maafisa wa serikali wawe na utayari na uelewa wa sheria zinazolinda haki ya mtoto katika jamii ili kutoyafumbua macho maovu kwa kisingizio cha kukosa ushirikiano wa wazazi na jamii, maana sharia iko wazi kuhusu uwajibishwaji kwa mtuhumiwa mara anapobainika na kosa. 
2.    Ni muhimu wa viongozi wa chama ambao tunaisimamia serikali katika utekelezaji wa ilani kuwa mtari wa mbele kukemea na kuhakikisha heria inafuta mkondo wake huku tukihamasisha wananchi kufuatilia haki zao za msingi kuliko kulalamika.
3.    Shule zote ziwekewe uzio ili kupunguza uvamizi wa  ardhiunaojitokeza mara kwa mara hasa katika shule ya Makuburi, Mabibo, makoka msingi na sekondari.


MALENGO
1. Jumuiya ya wazazi imekusudia kuwa na mfuko wa Elimu ambao utanufaisha vijana waliohitimu elimu ya sekondari na kushindwa kujiendeleza katika chuo cha ufundi VETA

2.  Kuunganisha wanachama na Saccos ya Mburahati na hatimaye kuwa na tawi ili kujenga umoja na baina ya Jumuiya za wazazi kata hata wilaya


HITIMISHO
KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI
UCHUNGU WA MWANA AUJUAE MZAZI


Imethibitishwa na kamati ya utekelezaji ya Baraza kuu la Wazazi kata ya Makuburi


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

VIONGOZI WA JUMUIYA YA WAZAZI

Na Voina Maganda JUMUIYA ya umoja wa wazazi ni chombo kinachoongozwa na chama cha Mapinduzi, kimeundwa kwa mujibu wa katiba ya Chama Cha M...