MWENYEKITI wa jumuiya ya wazazi Ndugu Justus Sangu amesisitiza ushirikiano na umuhimu wa semina kwa watendaji wa kata ili kuongeza ufanisi katika utekelezaji wa majukumu ya jumuiya na chama kwa ujumla katika kikao cha maandalizi ya semina ya Wazazi wilaya, leo katika ukumbi mdogo wa ofisi ya wilaya Kimara.
MWENYEKITI WA JUMUIYA YA WAZAZI NDUGU JASTUS SANGU AKISISITIZA JAMBO
(PICHA NA SWEDY MAKOYE)
Katika kikao hicho alikuwa pamoja na katibu wa Elimu, Malezi na Mazingira Ndugu King Mlanga ambaye naye alisisitiza katika kufikia malengo ya Jumuiya, kujali muda na maadili ya kazi katika kila hatua kwa kuzingatia uwazi na ushirikishwaji.
KATIBU EMMA WILAYA NDUGU KING MLANGA AKIONGEA JAMBO
Aidha katika kikao hicho wajumbe walikuwa ni watendaji wote wa jumuiya kutoka kata ambao ni katibu wa jumuia na katibu wa EMMA kutoka katika kata 14 zilizopo katika wilaya la Ubungo.
VIONGOZI WA WILAYA WAKISIKIZA MAONI YA WAJUMBE KWA MAKINI
Ubungo ni wilaya yenye kata 14, huku kata nne (4) zikiwa na madiwani wa CCM, tarafa mbili, majimbo mawili yakiwa na wabunge wa upinzani, serikali za mtaa 91, mitaa 64 ikiongozwa na Chama Cha Mapinduzi na matawi 137.
WAJUMBE WA KIKAO WAKICHANGIA HOJA
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni