Wanaofuata

Jumatatu, 7 Januari 2019

UMUHIMU WA JUMUIYA YA WAZAZI CHAMA





Jumuiya ya Wazazi ni moja kati ya jumuiya tatu ambazo ni nguzo ya Chama Cha Mapinduzi ambapo kila Jumuiya imebeba majukumu yake kwa lengo la kukisaidia chama kutekeleza Ilani ambayo imelenga kutatua kero na changamoto za wananchi katika nyanja zote za maendeleo.



Jumuiya hii ndiyo inasimamia Elimu, Malezi na Mazingira katika chama na mratibu mkuu wa shughuli hizi ni katibu wa Elimu, Malezi na Mazingira (KATIBU EMMA)

MAJUKUMU YA KATIBU WA ELIMU, MALEZI NA MAZINGIRA KATIKA JUMUIYA





KATIBU wa Elimu, Malezi na Mazingira wa wilaya Ndugu King Mlanga akifafanua umuhimu wa uwajibikaji kwa viongozi na matokeo chanya katika wilaya ya Ubungo


SIKU YA KWANZA OFISINI, KATIBU WA CHAMA WILAYA YA UBUNGO

Ijumaa, 4 Januari 2019

MAANDALIZI YA SEMINA JUMUIYA YA WAZAZI WILAYA YA UBUNGO

Na Voina Maganda

MWENYEKITI  wa jumuiya ya wazazi Ndugu Justus Sangu amesisitiza ushirikiano na umuhimu wa semina kwa watendaji wa kata ili kuongeza ufanisi katika utekelezaji wa majukumu ya jumuiya na chama  kwa ujumla katika kikao cha maandalizi ya semina ya Wazazi wilaya, leo  katika ukumbi mdogo wa ofisi ya wilaya Kimara.

MWENYEKITI WA JUMUIYA YA WAZAZI NDUGU JASTUS SANGU AKISISITIZA JAMBO
(PICHA NA SWEDY MAKOYE)


Sangu alianza na umuhimu wa kutumikia nafasi moja ili kuongeza ufanisi na uwajibikaji kwa watendaji wa Jumuiya, huku akisisitiza nidhamu na kufuata kanuni.

Katika kikao hicho alikuwa pamoja na katibu wa Elimu, Malezi na Mazingira Ndugu King Mlanga ambaye naye alisisitiza katika kufikia malengo ya Jumuiya, kujali muda na maadili ya kazi katika kila hatua kwa kuzingatia uwazi na ushirikishwaji.

KATIBU EMMA WILAYA NDUGU KING MLANGA AKIONGEA JAMBO 

Aidha katika kikao hicho wajumbe walikuwa ni watendaji wote wa jumuiya kutoka kata ambao ni katibu wa jumuia na katibu wa EMMA kutoka katika kata 14 zilizopo katika wilaya la Ubungo.

VIONGOZI WA WILAYA WAKISIKIZA MAONI YA WAJUMBE KWA MAKINI

Ubungo ni wilaya yenye kata 14, huku kata nne (4) zikiwa na madiwani wa CCM, tarafa mbili, majimbo mawili yakiwa na wabunge wa upinzani, serikali za mtaa 91, mitaa 64 ikiongozwa na Chama Cha Mapinduzi na matawi 137.

WAJUMBE WA KIKAO WAKICHANGIA HOJA 

MATUKIO KATIKA PICHA




KATIBU WA SIASA NA ORGANIZATION NDUGU CHOLLAGE ALLY (WA PILI KUTOKA KULIA) AKIPOKELEWA NA KAMATI YA UTEKELEZAJI WILAYA YA UBUNGO IKIONGOZWA NA MWENYEKITI WA WAZAZI (W) NDUGU JUSTUS SANGU (WA TATU KUTOKA KUSHOTO) KWA AJILI YA KUFUMGA KIKAO CHA BARAZA LA WILAYA KILICHOKAA 28/12/2018, UKUMBI WA DOLPHIN SINZA



KATIBU WA ELIMU, MALEZI NA MAZINGIRA WILAYA YA UBUNGO NDUGU KING (KULIA), KOMRED CHOLLAGE ALLY (KATIKATI) NA MWENYEKITI WA JUMUIYA YA WAZAZI (W) NDUGU JUSTUS SANGU, WAKIWA NA WAJUMBE WA KAMATI YA UTEKELEZAJI WILAYA KATIKA PICHA  YA PAMOJA




NDUGU CHOLLAGE ALLY AKIFUNGA KIKAO CHA BARAZA LA WAZAZI KWA KUSISITIZA UMUHIMU WA JUMUIYA YA WAZAZI KUTODIRIKI KUWA MADALALI WA WAGOMBEA WAKATI WA UCHAGUZI NA KUZINGATIA WAJIBU WA JUMUIYA KATIKA CHAMA NA JAMII AMBAO NI ELIMU, MALEZI NA MAZINGIRA (PICHA ZOTE KWA HISANI YA MAKOYE)

VIONGOZI WA JUMUIYA YA WAZAZI

Na Voina Maganda JUMUIYA ya umoja wa wazazi ni chombo kinachoongozwa na chama cha Mapinduzi, kimeundwa kwa mujibu wa katiba ya Chama Cha M...