Wanaofuata

Jumatano, 9 Januari 2019

OFISI ZA TAWI LA MAVURUNZA ZAKARABATIWA

Na Voina Maganda

MJUMBE wa kamati ya utekelezaji wa Jumuiya ya wazazi Rose Patrick Kazonda wa kata ya Kimara, tawi la Mavurunza akarabati ofisi za tawi zilizopo eneo hilo bila masharti ya aina yeyote na kuzikabidhi kutokana na ushirikiano mzuri uliopo kati ya viongozi wa chama, wananchi na serikali.

Ukarabati huo wa vyumba viwili ambao ulichukua muda wa miezi mitatu, unakadiliwa kugharimu kiasi cha Tshs 8,000,000/=  (Milioni Nane) ambao ulikuwa wa kusakafia upya, kuziba mipasuko, kupaka rangi, kubadilisha madirisha kuweka ya Aluminiumu na kuweka dali (ceilling board).


COMRED ROSE PATRICK KAZONDA AKIWA MBELE YA OFISI ZA TAWI LA MAVURUNZA LEO ALIPOFIKA KWENYE ZIARA YA CHAMA


Akiongea na mwandishi wa blog ya CCMWAZAZI mbele ya ofisi cha tawi hilo Kazonda alisema kuwa alisukumwa na mapenzi aliyonayo katika chama, Uongozi wa Taifa wa serikali na kuamua kuunga mkono juhudi za chama katika kurejesha imani za wananchi kwa serikali yao.

KUTOKA KUSHOTO NI KAIMU KATIBU WA KATA YA KIMARA NA KATIBU WA JUMUIYA YA WAZAZI MWAJUMA MLUNGILA, ROSE PATRICK KAZONDA MJUMBE WA KAMATI YA UTEKELEZAJI KATA (WAZAZI), MWENYEKITI WA TAWI LA MAVURUNZA CHAMA GAIDON LUKUI, NA MWENYEKITI WA KATA YA KIMARA CHAMA BILALI RAJABU WAKIWA MBELE YA OFISI YA TAWI LA MAVURUNZA

"Mimi kama mwanachama wa CCM, nilijiuliza nimefanya nini kwa ajili ya chama changu na nchi yangu, maana CCM ndio wenye Ilani na watendaji wake hawana ofisi nzuri itakayowafanya watekeleze majukumu yao katika kuisimamia Ilani, ndipo likaja wazo la kukarabati ofisi hizo", alisema Kazonda.

Aidha Kazonda alikabidhi jengo hilo tarehe 02/08/2018 kwa uongozi wa Tawi hilo ukiongozwa na mwenyekiti Gidion Lukui, ukishuhudiwa na viongozi wa kata na kamati zote zilizomo ndani ya chama na siku hiyo ndiyo ofisi uliyotumika kumuapika Diwani Paschal Manota aliyepita bila kupingwa baada ya kujitoa uanachana wa CHADEMA.
KUTOKA KUSHOTO DIWANI WA KATA YA KIMARA COMRED PASCHAL MANOTA, MWENYEKITI WA TAWI LA MAVURUNZA CHAMA GAIDON LUKUI, NA MWENYEKITI WA KATA YA KIMARA CHAMA BILALI RAJABU KWENYE VIWANJA VYA OFISI YA TAWI LA MAVURUNZA WAKIBADILISHANA MAWAZO

Sikutegemea kulipwa chochote, nilifanya ukarabati kwa hiari yangu, na sasa najisikia amani na furaha tawi hili kuwa na ofisi nzuri, aliongeza Kazonda.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

VIONGOZI WA JUMUIYA YA WAZAZI

Na Voina Maganda JUMUIYA ya umoja wa wazazi ni chombo kinachoongozwa na chama cha Mapinduzi, kimeundwa kwa mujibu wa katiba ya Chama Cha M...