KATIBU WA SIASA NA UENEZI WILAYA YA UBUNGO COMRED MBARUKU MASOUD MOHAMED ALIYESIMAMA AKITOA MAELEKEZO KATIKA ZIARA YA KAMATI NA SEKRETARIETI YA KATA YA KIMARA
KATIBU wa Siasa na Uenezi Wilaya ya Ubungo Ndugu MBARUKU MASOUD MOHAMED amekumbushia mambo makubwa manne aliyowaagiza viongozi wa Chama Kata wakayatekeleze katika kata zao leo kwenye uwanja uliopo nyuma ya ofisi za tawi la Mavurunza, katika Ziara ya Kamati ya siasa na sekretarieti ya kata iliyohusisha mashina manne yaliyoko katika tawi la Mavurunza.
Maagizo yalikuwa ni
1. Viongozi wa kata wahakikishe wanafanya ziara kwenye mashina ili kufanya uhakiki na kujua uhai wa wanachama.
2. Kuwaandaa wanachama na uchaguzi wa mwaka 2019 ambao utakuwa ni wa serikali ya mtaa huku akitoa taadhara ya kutoanza klampeni kabla muda wa muda wake.
3. Kuhimiza wanachama kusajiliwa kwa njia ya kieletronic ni kupata kadi mpya za kisasa ambazo ndizo zitatumika ili kuwa na uhakika na idadi ya wanachama waliopo maana uitikio ulikuwa mdogo wakati zoezi hilo likifanyika katika kata hiyo.
4. Kubaini na kutambua changamoto zilizopo katika kata hiyo ili kuzitafutia uvumbuzi wa haraka
Aidha hakusita kumpongeza Diwani wa Kata hiyo Mh. Paschal Manota kuwa ndiye Diwani pekee kati ya madiwani wanne waliopo Wilaya ya Ubungo wanaotokana na CCM ambaye anaitendea haki nafasi yake.
"Sio siri na wala sitasita kuliongea hili hata madiwani wengine wakiwepo, wewe Ndugu Manota ndiye Diwani pekee unaeitendea haki nafasi yako, na hata ulipokuwa kule (CHADEMA) naelewa walikutegemea kwa kiasi kikubwa sana, kuwa na amani, yale ambayo yatakuwa nje ya uwezo wako tuletee tutasaidiana kuyatatua" alisema Mbaruku.
Mbaruku aliongeza kuwa Tawi la Mavurunza ni kati ya matawi ambao yana mwamko wa kisiasa pia ina wanachama ambao wanautendea haki uanachama wao na hayo yote yanadhihirishwa katika kuitikia wito mara waitwapo kwenye mikutano ya chama.
Hata hivyo wanachama walitoa kero zao ambazo zimekuwa zikijirudia mara kwa mara katika tawi hilo ambazo ni miundombinu mibovu hasa barabara ambayo husababisha huduma ya kuzoa taka kutowafikia walengwa walioko eneo ambalo gari haliwezi kufika, wajumbe wa mashina kutotoa ushirikiano kwa wananchi hasa kama hajapewa chochote, kutopatikana kwa muda kwa kadi za chama.
Wananchi katika maoni yao walishauri chama kuhakikisha kinawawezesha mabolozi vitendea kazi ili wananchi wapate huduma kwa urahisi na kupunguza au kuondoa kabisa tabia ya mabolozi kuomba pesa za huduma kwa wananchi.
Hapo kabla Mbaruku alihimiza Upendo, Umoja na Mshikamano kati ya viongozi na viongozi, viongozi na wanachama maana hizo ndizo nguzo za kukifanya Chama cha Mapinduzi kuendelea kuwa na nguvu dhidi ya vyama vya upinzani kwa kuendelea kushinda kila chaguzi.
"Imekuwa tabia kuwepo kwa migawanyika inapokaribia wakati wa uchaguzi jambo ambalo linasababishwa na kukosekana kwa upendo, umoja na mshikamano, ni lazima tubadilike ili kufikia malengo tuliyojipangia" amesema Mbaruku.
Diwani Paschal Manota akijibu baadhi ya hoja za katibu Siasa na uenezi Mbaruku, aliahidi kushirikiana na uongozi wa kata ya Kimara kuhakikisha mitaa yote sita inaongozwa na Chama Cha Mapinduzi kwenye uchaguzi ujao wa serikali za mtaa utakaofanyika mapema mwaka huu.
KATIBU WA SIASA NA UENEZI WILAYA MBARUKU MASOUD MOHAMED AKIONYESHA MFANO WA KADI ZA KIELECTRONIC
Aidha Manota alimpongeza Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Mh. John Pombe Joseph Magufuli kwa utekelezaji wa Ilani ambao hauitaji jicho la ziada kuweza kuuona na kutambua mambo mazuri aliyoyasimamia kwa manufaa ya Taifa.
"Unajua ukiwa upande ule unakosa ufahamu kabisa akili yako inakuwa ni kupinga tu ili kujitutumua kwa wananchi, lakini kwa Rais huyu hata ujifanye huoni ni lazima tukiri kuwa anafanya kazi aliyotumwa na wananchi." alisema.
Aliongeza kuwa, wakati wa kuweka jiwe la msingi la barabara ya Morogoro pale Kimara alitegemea viongozi wa pande zile yaani CHADEMA kuomba barabara inayotoka kimara mwisho kuelekea Bonyokwa iwekewe rami ili ujenzi wa barabara Nane uwe na faida zaidi kwa wakazi na watumiaji wa barabara ile wenyewe wanataka demokrasia, kwani demokrasia haipo?
Manota hakusita kuongelea mradi ya maji ya kilomita 7 unaotokea Kimara mwisho na mradi wa kilomita 3.58 ambao umefikia katika hatua nzuri na wakati wowote mwaka huu wananchi wa kata ya Kimara watanufaika nao, japo maji yapo lakini kutakuwa na maji ya kutosha.
Katika ziara hiyo Katibu Muenezi Mbaruku alipokea wanachama wapya 80 kutoka katika tawi la Mavurunza. Mashina ya tawi hilo ni shina namba 7,8,11 na 16 ambayo ni baadhi tu ya mashina 123 yakiyopo katika kata ya Kimara.
KATIBU WA SIASA NA UENEZI WILAYA MBARUKU MASOUD MOHAMED AKIAPISHA WANACHAMA WAPYA KABLA YA KUTOA KADI
MMOJA WA WANACHAMA WAPYA AKIPOKEA KADI YA UANACHAMA
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni