Wanaofuata

Ijumaa, 11 Januari 2019

VIONGOZI WA JUMUIYA YA WAZAZI

Na Voina Maganda
JUMUIYA ya umoja wa wazazi ni chombo kinachoongozwa na chama cha Mapinduzi, kimeundwa kwa mujibu wa katiba ya Chama Cha Mapinduzi, ya mwaka 1977 Toleo la mwaka 2012 sehemu ya nne ibara ya 129 (1c), 3,4, na 5.

Jumuiya hii ina viongozi kuanzia ngazi ya Taifa mpaka matawi, wilaya ya Ubungo ina kata 14, matawi 137 ambayo yana viongozi na kamati za utekelezaji ambazo zina jukumu la kujadili na kufanya maamuzi yanayohusiana na Jumuiya.

MWENYEKITI WAZAZI MKOA WA DAR ES SALAAM COMRED FRANK KAMGISHA KUSHOTO NA KATIBU MKUU WAZAZI TAIFA COMRED ERASTO SIMA WAKIFUATILIA JAMBO SIKU YA BARAZA LA WAZAZI KATA MBURAHATI (29/12/2018) PICHA NA ALHAJI  MAKOYE

 KATIBU WAZAZI MKOA DAR ES SALAAM COMRED LUGANO MWAFONGO AKIONGEA JAMBO SIKU YA BARAZA LA WAZAZI KATA MBURAHATI (29/12/2018)


 MMOJA WA WANACHAMA ALIJIUNGA NA JUMUIYA YA WAZAZI KATI WANACHAMA 380 WAPYA, KADI HIZO ZILITOLEWA NA KATIBU MKUU WAZAZI TAIFA COMRED ERASTO SIMA BAADA YA KUWAAPISHA

COMRED FRANK KAMUGISHA AKITOA NENO NA UKARIBISHO KWA VIONGOZI 

 KATIBU ELIMU, MALEZI NA MAZINGIRA WILAYA YA UBUNGO KING RASHID MLANGA AKITAMBULISHA VIONGOZI WA WILAYA KWA WAGENI
 WANACHAMA WA CCM NA JUMUIYA KUTOKA MATAWI MANNE YALIYOKO KATA YA MBURAHATI WAKISIKILIZA NENO KUTOKA KWA VIONGOZI

MMOJA WA WANACHAMA ALIJIUNGA NA JUMUIYA YA WAZAZI KATI WANACHAMA 380 WAPYA, KADI HIZO ZILITOLEWA NA KATIBU MKUU WAZAZI TAIFA COMRED ERASTO SIMA BAADA YA KUWAAPISHA
MWENYEKITI WAZAZI WILAYA COMRED JASTUS SANGU KULIA NA MWENYEKITI WAZAZI KATA YA MBURAHATI COMRED JOHN EXAVERY MAPUNDA WAKITETA JAMBO

KATIBU MKUU WAZAZI TAIFA COMRED ERASTO SIMA AFUNGA MWAKA 2018 NA BAR...



KATIBU Mkuu Jumuiya ya Wazazi Taifa Erasto Sima afunga mwaka na Mkutano wa Baraza la Wazazi kata ya Mburahati kwa kuhimiza umuhimu wa wanachama kujisajili kwa njia ya kielectonic zoezi ambalo limeeshaanza.

RAHA YA SIASA KWA MWENYE SIASA



KATIBU wa siasa na uenezi wilaya ya Ubungo Mbaruku Masoud Mohamed asisitiza umuhumu wa viongozi kuwajibika na kufuata maelekezo kwa wakati.

Jumatano, 9 Januari 2019

DIWANI MANOTA ATOBOA SIRI YA KUNOGA KWAKE

Na Voina Maganda

DIWANI wa kata Kimara, wilaya ya Ubungo (Jana) Paschal Manota atamba kunoga baada ya kujiunga Chama cha Mapinduzi leo katika ziara ya kamati ya siasa na sekretarieti ya kata katika mashina manne ya tawi la Mavurunza.
DIWANI WA KATA YA KIMARA PASCHAL MANOTA WA PILI KUSHOTO AKIWA NA VIONGOZI WA KATA NA TAWI LA MAVURUNZA (SWEDY MAKOYE)

Akiongea kwa mbwembwe alisema "siku hizi imekuwa ada kila anapopita anaambiwa na wananchi kuwa kanoga yaani anang'aa na kupendeza nami huwa nawajibu niko mahali salama ambako hakuna stress aka (free stress zone)".

Ukiwa upinzani unakosa ufahamu hata sielewi ni jambo gani huwa linatukumba maana kazi ni kupinga tu kila kitu bila kujali unachopinga, unakuwa na upofu fulani na unalazimika kujitoa ufahamu, aliongeza Manota.

Hata hivyo Manota hakusita kushukuru wanachama na viongozi kwa ushirikiano na mapokezi mazuri anayopata na hali hiyo imemfanya kuwa na amani.

Manota ni mmoja wa madiwani wa nne waliopo Ubungo kwa tiketi ya CCM.

MOTO WA KATIBU SIASA NA UENEZI WILAYA UBUNGO SI MCHEZO

KATIBU WA SIASA NA UENEZI WILAYA YA UBUNGO COMRED MBARUKU MASOUD MOHAMED ALIYESIMAMA AKITOA MAELEKEZO KATIKA ZIARA YA KAMATI NA SEKRETARIETI YA KATA YA KIMARA 


Na Voina Maganda
KATIBU wa Siasa na Uenezi Wilaya ya Ubungo Ndugu MBARUKU MASOUD MOHAMED amekumbushia mambo makubwa manne aliyowaagiza viongozi wa Chama Kata wakayatekeleze katika kata zao leo kwenye uwanja uliopo nyuma ya ofisi za tawi la Mavurunza, katika Ziara ya Kamati ya siasa na sekretarieti ya kata iliyohusisha mashina manne yaliyoko katika tawi la Mavurunza.

Maagizo yalikuwa ni
1. Viongozi wa kata wahakikishe wanafanya ziara kwenye mashina ili kufanya uhakiki na kujua uhai wa wanachama.

2. Kuwaandaa wanachama na uchaguzi wa mwaka 2019 ambao utakuwa ni wa serikali ya mtaa huku akitoa taadhara ya kutoanza klampeni kabla muda wa muda wake.

3. Kuhimiza wanachama kusajiliwa kwa njia ya kieletronic ni kupata kadi mpya za kisasa ambazo ndizo zitatumika ili kuwa na uhakika na idadi ya wanachama waliopo maana uitikio ulikuwa mdogo wakati zoezi hilo likifanyika katika kata hiyo.

4. Kubaini na kutambua changamoto zilizopo katika kata hiyo ili kuzitafutia uvumbuzi wa haraka


Aidha hakusita kumpongeza Diwani wa Kata hiyo Mh. Paschal Manota kuwa ndiye Diwani pekee kati ya madiwani wanne waliopo Wilaya ya Ubungo wanaotokana na CCM ambaye anaitendea haki nafasi yake.

"Sio siri na wala sitasita kuliongea hili hata madiwani wengine wakiwepo, wewe Ndugu Manota ndiye Diwani pekee unaeitendea haki nafasi yako, na hata ulipokuwa kule (CHADEMA) naelewa walikutegemea kwa kiasi kikubwa sana, kuwa na amani, yale ambayo yatakuwa nje ya uwezo wako tuletee tutasaidiana kuyatatua" alisema Mbaruku.

Mbaruku aliongeza kuwa Tawi la Mavurunza ni kati ya matawi ambao yana mwamko wa kisiasa pia ina wanachama ambao wanautendea haki uanachama wao na hayo yote yanadhihirishwa katika kuitikia wito mara waitwapo kwenye mikutano ya chama.

Hata hivyo wanachama walitoa kero zao ambazo zimekuwa zikijirudia mara kwa mara katika tawi hilo ambazo ni miundombinu mibovu hasa barabara ambayo husababisha huduma ya kuzoa taka kutowafikia walengwa walioko eneo ambalo gari haliwezi kufika, wajumbe wa mashina kutotoa ushirikiano kwa wananchi hasa kama hajapewa chochote, kutopatikana kwa muda kwa kadi za chama.

Wananchi katika maoni yao walishauri chama kuhakikisha kinawawezesha mabolozi vitendea kazi ili wananchi wapate huduma kwa urahisi na kupunguza au kuondoa kabisa tabia ya mabolozi kuomba pesa za huduma kwa wananchi.

Hapo kabla Mbaruku alihimiza Upendo, Umoja na Mshikamano kati ya viongozi na viongozi, viongozi na wanachama maana hizo ndizo nguzo za kukifanya Chama cha Mapinduzi kuendelea kuwa na nguvu dhidi ya vyama vya upinzani kwa kuendelea kushinda kila chaguzi.

"Imekuwa tabia kuwepo kwa migawanyika inapokaribia wakati wa uchaguzi jambo ambalo linasababishwa na kukosekana kwa upendo, umoja na mshikamano, ni lazima tubadilike ili kufikia malengo tuliyojipangia" amesema Mbaruku.

Diwani Paschal Manota akijibu baadhi ya hoja za katibu Siasa na uenezi Mbaruku, aliahidi kushirikiana na uongozi wa kata ya Kimara kuhakikisha mitaa yote sita inaongozwa na Chama Cha Mapinduzi kwenye uchaguzi ujao wa serikali za mtaa utakaofanyika mapema mwaka huu.

KATIBU  WA SIASA NA UENEZI WILAYA MBARUKU MASOUD MOHAMED AKIONYESHA MFANO  WA KADI ZA KIELECTRONIC

Aidha Manota alimpongeza Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Mh. John Pombe Joseph Magufuli kwa utekelezaji wa Ilani ambao hauitaji jicho la ziada kuweza kuuona na kutambua mambo mazuri aliyoyasimamia kwa manufaa ya Taifa.

"Unajua ukiwa upande ule unakosa ufahamu kabisa akili yako inakuwa ni kupinga tu ili kujitutumua kwa wananchi, lakini kwa Rais huyu hata ujifanye huoni ni lazima tukiri kuwa anafanya kazi aliyotumwa na wananchi." alisema.

Aliongeza kuwa, wakati wa kuweka jiwe la msingi la barabara ya Morogoro pale Kimara alitegemea viongozi wa pande zile yaani CHADEMA kuomba barabara inayotoka kimara mwisho kuelekea Bonyokwa iwekewe rami ili ujenzi wa barabara Nane uwe na faida zaidi kwa wakazi na watumiaji wa barabara ile wenyewe wanataka demokrasia, kwani demokrasia haipo?

Manota hakusita kuongelea mradi ya maji ya kilomita 7 unaotokea Kimara mwisho na mradi wa kilomita 3.58 ambao umefikia katika hatua nzuri na wakati wowote mwaka huu wananchi wa kata ya Kimara watanufaika nao, japo maji yapo lakini kutakuwa na maji ya kutosha.

Katika ziara hiyo Katibu Muenezi Mbaruku alipokea wanachama wapya 80 kutoka katika tawi la Mavurunza. Mashina ya tawi hilo ni shina namba 7,8,11 na 16 ambayo ni baadhi tu ya mashina 123 yakiyopo katika kata ya Kimara. 
KATIBU  WA SIASA NA UENEZI WILAYA MBARUKU MASOUD MOHAMED AKIAPISHA WANACHAMA WAPYA KABLA YA KUTOA KADI

MMOJA WA WANACHAMA WAPYA AKIPOKEA KADI YA UANACHAMA

OFISI ZA TAWI LA MAVURUNZA ZAKARABATIWA

Na Voina Maganda

MJUMBE wa kamati ya utekelezaji wa Jumuiya ya wazazi Rose Patrick Kazonda wa kata ya Kimara, tawi la Mavurunza akarabati ofisi za tawi zilizopo eneo hilo bila masharti ya aina yeyote na kuzikabidhi kutokana na ushirikiano mzuri uliopo kati ya viongozi wa chama, wananchi na serikali.

Ukarabati huo wa vyumba viwili ambao ulichukua muda wa miezi mitatu, unakadiliwa kugharimu kiasi cha Tshs 8,000,000/=  (Milioni Nane) ambao ulikuwa wa kusakafia upya, kuziba mipasuko, kupaka rangi, kubadilisha madirisha kuweka ya Aluminiumu na kuweka dali (ceilling board).


COMRED ROSE PATRICK KAZONDA AKIWA MBELE YA OFISI ZA TAWI LA MAVURUNZA LEO ALIPOFIKA KWENYE ZIARA YA CHAMA


Akiongea na mwandishi wa blog ya CCMWAZAZI mbele ya ofisi cha tawi hilo Kazonda alisema kuwa alisukumwa na mapenzi aliyonayo katika chama, Uongozi wa Taifa wa serikali na kuamua kuunga mkono juhudi za chama katika kurejesha imani za wananchi kwa serikali yao.

KUTOKA KUSHOTO NI KAIMU KATIBU WA KATA YA KIMARA NA KATIBU WA JUMUIYA YA WAZAZI MWAJUMA MLUNGILA, ROSE PATRICK KAZONDA MJUMBE WA KAMATI YA UTEKELEZAJI KATA (WAZAZI), MWENYEKITI WA TAWI LA MAVURUNZA CHAMA GAIDON LUKUI, NA MWENYEKITI WA KATA YA KIMARA CHAMA BILALI RAJABU WAKIWA MBELE YA OFISI YA TAWI LA MAVURUNZA

"Mimi kama mwanachama wa CCM, nilijiuliza nimefanya nini kwa ajili ya chama changu na nchi yangu, maana CCM ndio wenye Ilani na watendaji wake hawana ofisi nzuri itakayowafanya watekeleze majukumu yao katika kuisimamia Ilani, ndipo likaja wazo la kukarabati ofisi hizo", alisema Kazonda.

Aidha Kazonda alikabidhi jengo hilo tarehe 02/08/2018 kwa uongozi wa Tawi hilo ukiongozwa na mwenyekiti Gidion Lukui, ukishuhudiwa na viongozi wa kata na kamati zote zilizomo ndani ya chama na siku hiyo ndiyo ofisi uliyotumika kumuapika Diwani Paschal Manota aliyepita bila kupingwa baada ya kujitoa uanachana wa CHADEMA.
KUTOKA KUSHOTO DIWANI WA KATA YA KIMARA COMRED PASCHAL MANOTA, MWENYEKITI WA TAWI LA MAVURUNZA CHAMA GAIDON LUKUI, NA MWENYEKITI WA KATA YA KIMARA CHAMA BILALI RAJABU KWENYE VIWANJA VYA OFISI YA TAWI LA MAVURUNZA WAKIBADILISHANA MAWAZO

Sikutegemea kulipwa chochote, nilifanya ukarabati kwa hiari yangu, na sasa najisikia amani na furaha tawi hili kuwa na ofisi nzuri, aliongeza Kazonda.

MAADHIMISHO YA MWAKA MMOJA WILAYA UBUNGO





Mwenyekiti wa Chama Wilaya Comrade Lucas Mgonja, asisitiza Upendo, Umoja na Mshikamano siku ya maadhimisho mwaka mmoja tokea kusimikwa kwa uongozi wa chama.

Ubungo ni miongoni mwa wilaya tano mkoani Dar es Salaam.

VIONGOZI WA JUMUIYA YA WAZAZI

Na Voina Maganda JUMUIYA ya umoja wa wazazi ni chombo kinachoongozwa na chama cha Mapinduzi, kimeundwa kwa mujibu wa katiba ya Chama Cha M...